loader
Utafiti mbolea asilia  mbioni kusaidia wakulima

Utafiti mbolea asilia mbioni kusaidia wakulima

TAASISI ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, imekuwa mstari wa mbele kutoa elimu inayolenga kusaidia jamii na kukuza viwanda kupitia tafiti na ubunifu unaofanywa na wanafunzi wa taasisi hiyo.

Hayo yamejidhihirisha kupitia mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Kilimo Endelevu wa Taasisi hiyo, Monica Nakei,  ambaye anafanya utafiti wa mbolea asilia itokanayo na vimelea vya bakteria jamii ya rhizobia.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, iliyotolewa leo Agosti 5, 2022, inasema kuwa mwanafunzi huyo amefanya utafiti wa mbolea hiyo kupitia zao la soya na kwamba utafiti ukatapokamilika, mbolea hiyo itakuwa tayari kwa matumizi.

Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, utafiti wake amegundua kuwa mbolea hiyo ina faida nyingi ikiwemo kuongeza virutubisho vya nitrogeni na fosforasi kwa mimea ya soya na kuimarisha afya ya udongo na kuweka usawa katika mfumo wa ikolojia ya udongo.

Amesema faida nyingine ni pamoja na mazao yatokanayo na mbolea hiyo, kutokuwa na kemikali zenye kuleta madhara kwa walaji na gharama yake ni nafuu kwa wakulima.

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, inashiriki maonesho ya 28 ya Nanenane yanayoendelea  katika  viwanja vya Themi jijini Arusha, ambapo kupitia wanafunzi wake inaendelea kutoa elimu mbalimbali kuhusu kilimo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/751f47edeaba47327b2813dc60fbf196.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi