loader
DC Sumbawanga ataka wananchi washiriki sensa

DC Sumbawanga ataka wananchi washiriki sensa

MKUU wa Wilaya ya Sumbawanga, Sebastian Waryuba, amewataka wananchi kujitokeza kikamilifu kushiriki  sensa kwa lengo la kuirahisishia serikali kupanga mipango mbalimbali ya kimaendeleo Agosti 23 mwaka huu.

Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya hiyo, amesema Rais Samia Suluhu Hassan ana malengo mazuri kwa Watanzania, hivyo hakuna budi kushiriki sensa hiyo, kwani ni njia mojawapo kuiwezesha serikali kufikia malengo yake.

"Niwaase viongozi wenzangu kujitokeza kwa wingi na kuwahamasisha wananchi wetu kushiriki sense, kama ambavyo Rais Samia na viongozi wengine wa ngazi za juu wanavyotuhamasisha, kwa pamoja tunaweza kufanikisha hilo," amesema Waryuba na kuongeza:

 

"Tunawaomba wananchi wote bila kujali imani zetu na itikadi zetu ni vyema kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika sensa hii ya watu na makazi, hii itasaidia serikali yetu kufahamu idadi kamili ya wananchi wake na hivyo kuweka mipango yake ya kuwahudumia," amesema Waryuba.

Pia atika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya, amesema tangu Rais Samia aingie madarakani kuiongoza Serikali ya Awamu ya Sita, ameonesha dira katika masuala mbalimbali ya kiuchumi na kimaendeleo, hali iliyosaidia kuongeza idadi ya wawekezaji kuja nchini.

"Leo hii tunaona kwa macho yetu namna idadi kubwa ya watalii wanaoingia nchini, hili limetokana na wazo lake la kuja na filamu ya Royal Tour, ambayo kimsingi imeongeza chachu ya watalii kutoka mataifa mbalimbali kuja kuitembelea Tanzania," amesisitiza Waryuba.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/785e2a01b90191c80c1cda6571608ceb.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi