loader
Wakulima wazuia malori, wadai kutapeliwa

Wakulima wazuia malori, wadai kutapeliwa

WAKULIMA  wa mahindi zaidi ya 150 wameshikilia malori matano na tela za mfanyabiashara maarufu nchini Kenya Erick Kimati, yakiwa na mzigo wa mahindi tani 1,500, wakidai ameshindwa kuwalipa fedha zao.

Mfanyabiashara huyo anadaiwa kununua mahindi tani 600 kutoka kwa wakulima hao kwa mali kauli.

Malori yaliyokamatwa mali ya kampuni ya usafirishaji ya Joy Miller’s ya nchini Kenya ni yenye namba za usajili KDH047R tela lake limesajiliwa kwa namba ZG8419, gari lingine lina namba za usajili KDC188M na tela namba ZF5730.

Pia lipo gari lenye namba za ZG8421 na tela namba KDH043R, gari lingine ZG046R tela lenye usajili ZD8420, pia kuna lori namba ZG8422 na  tela namba za usajili KDH045R malori yote yako katika ghala lililopo Kwa Murombo jijini Arusha.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake, Zainabu Ngosha kutoka Mwanza, amesema Kimati amekuwa akiwazungusha kulipa fedha zao tangu mwezi Juni, licha ya kumfuatilia mara kadhaa, lakini jitihada zao hazijazaa matunda.

Kufuatia hali hiyo, wakulima hao wamemwangukia Rais Samia Suhulu Hassan, ili aweze kuwasaidia na kudai kuwa hawajapata msaada kwa viongozi wa Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Said Mtanda alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, amesema Kenya na Tanzania wanaishi kwa kushirikiana kwa hali na mali na iwapo suala hilo litafika mezani kwake atalishughulikia.

 

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ceb2372ffee85ab261221aafb55f4a5a.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi