MKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela amewataka wataalamu kwenda kushughulikia kero za wananchi badala ya kutumia muda mwingi ofisini.
Shigela ameyasema hayo leo Agosti 5, 2022, baada ya kuripoti rasmi mkoani humo na kuzungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa.
Amesema kipaumbele chake kikubwa akiwa kiongozi wa mkoa ni kusikiliza, kushughulika na kutatua kero za wananchi, ili kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan.
Amesema ili kutatua kero za wananchi ni lazima wataalamu wa serikali na watumishi wa mkoa, waache tabia ya kufanya kazi zao ofisini muda wote na waende kwenye maeneo ya wananchi na kuondoa kero zao.
“Kikubwa ni kuwatumikia wananchi kushughulika na kero za wananchi na kusimamia fedha za mapato, ili kufikia maendeleo na katika kuhakikisha tunachagiza upatikanaji wa miradi yenye tija.
“Jitihada tulizozifanya mwaka jana, mikakati tuliyofanya tuweze kuiboresha zaidi ili tuhakikishe tunafikia hayo malengo tusishuke chini zaidi, tubuni vyanzo vipya vya mapato,” amesema.