loader
Dendego atoa maelekezo mapato Iringa

Dendego atoa maelekezo mapato Iringa

 MKUU wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego amekabidhiwa ofisi na mtangulizi wake, Queen Sendiga, mapema leo akiwataka wasaidizi wake kuzigeuza changamoto zote za mkoa huo kuwa fursa na kubuni vyanzo vipya vya mapato.

"Kwenye suala la mapato sitakuwa na mzaha. Nataka kuona mnakaza uzi kwenye makusanyo yenu na mnakuja na majawabu ya namna ya kuzishughulikia changamoto zinazowahusu wananchi wetu kwa maendeleo yao, mkoa na Taifa," amesema Dendego.

 Akiwaaga watumishi na wakazi wa mkoa wa Iringa, Sendiga alimkaribisha Dendego akisema mkoa wa Iringa una watu waungwana, wamemfunza na kumfanya mbobezi katika shughuli za kuwatumikia wananchi na akawataka wayaendeleze yote mazuri na kumpa ushirikiano mkuu wa mkoa mpya.

"Nimeyapokea mabadiliko kwa mikono miwili na kwa moyo mkunjufu, nakwenda Rukwa nikiwa na ari na nguvu kubwa. Nimuahidi Mheshimiwa Rais, ninakwenda kumsaidia kutekeleza majukumu ya kiserikali kikamilifu na kwa kasi kubwa," Sendiga alisema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/b31ff06b1455d19097a781e51abe5fcd.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Frank Leonard, Iringa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi