loader
Mfumo  udhibiti rasilimali za maji waanza kutumika

Mfumo udhibiti rasilimali za maji waanza kutumika

SERIKALI  imeanza rasmi matumizi ya  mfumo wa udhibiti ubora wa takwimu za rasilimali za maji (QMS), kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa bodi za maji za mabonde nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Wizara ya Maji, Simon Nkanyemka na kwamba  lengo kuu ni  kuboresha utendaji wa shughuli ya msingi za mabonde ya usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji kwa kutumia takwimu sahihi za wingi na ubora zitakazofanikisha kutimiza malengo ya serikali ya muda mfupi, kati na mrefu.

“Jukumu la msingi la Wizara ya Maji ni kusimamia sera na sheria katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji ya uhakika mijini na vijijini, jukumu ambalo litafanikiwa kuweka mikakati madhubuti ya usimamizi wa rasilimali za maji kwa kuwa na takwimu sahihi zitakazosaidia kutimiza malengo ya wizara,” amesema.

Amesema Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Ujerumani (GiZ), wanalenga kuimarisha eneo la ukusanyaji wa takwimu sahihi za hali ya maji, hatua itakayowawezesha mabonde yote yaweze kupata vyeti vya ithibati vya ubora utakaotokana ufanisi wa mabonde hayo.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Rasilimali za Maji Wizara ya Maji, Robert Sunday, amesema nyaraka 373 za QMS, zimeandaliwa na zimeanza kutumika rasmi pamoja na utekelezaji rasmi wa QMS kwa mabonde yote tisa nchini, ambayo ni Bodi za Maji za Mabonde ya Rufiji, Wami-Ruvu, Kati, Ruvuma na Pwani ya Kusini, Mto Pangani, Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa na Ziwa Nyasa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7b16c4b1e0d284e5481071f7d75fa302.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi