loader
Wabunge 21, watumishi wa Bunge wahitimu mafunzo JKT

Wabunge 21, watumishi wa Bunge wahitimu mafunzo JKT

WABUNGE 21 na watumishi wa Bunge 18, wamehitimu mafunzo yao kwa mujibu wa sheria kwa kundi maalum la taasisi hiyo yaliyodumu kwa muda wa mwezi mmoja.

Mafunzo hayo yaliyopewa jina la operesheni Jenerali Venance Mabeyo, yalifanyika katika kambi ya JKT Makutupora mkoani Dodoma, yalianza Julai 5 mwaka huu.

Akifunga mafunzo hayo leo Agosti 5, 2022 Mkuu wa Utumishi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Jenerali Paul Simuli, ameipongeza serikali kwa kuendelea kuwezesha mafunzo kwa mujibu wa sheria pamoja na kulishukuru Bunge kuwaruhusu watumishi wake kuhudhuria mafunzo hayo.

Meja Jenerali Simuli amewataka wahitimu hao kuwa mabalozi wa kutunza amani na umoja pamoja na kuendelea kuwa wazalendo kwa nchi, huku akizialika taasisi zingine kuweza kupata mafunzo hayo.

Kwa upande wake Katibu wa Bunge, ambaye pia alihudhuria kuhitimishwa kwa mafunzo hayo, Nenelwa Mwihambi ameahidi kuendelea kushirikiana na jeshi na kuhakikisha watumishi na wabunge wanapatiwa mafunzo hayo kwa ajili ya kuwajengea uzalendo, ukakamavu na ujasiri zaidi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e93dc007b45d78cd05d213911ebc8508.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Iddy Mwema, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi