loader
Kihenzile azindua kongamano la VIWAWA

Kihenzile azindua kongamano la VIWAWA

RAIS wa Red Cross Tanzania, ambaye pia ni Mbunge wa Mufindi Kusini, David Kihenzile amezindua Kongamano la tano la Taifa la Vijana Wakatoliki Wafanyakazi Tanzania (VIWAWA)

Uzinduzi wa Kongamano hilo la siku nne umefanyika katika viwanja vya Mtakatifu Theresia Mtoto wa Yesu, Jimbo Kuu la Tabora likiwa na kauli mbiu Simama Nimekuteua Uwe Shahidi wa Yale Uliyoyaona.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Kihenzile amesema, vijana  wanapokumbana na vikwazo katika imani au imani yao inapoanza kuyeyuka kama ndoto ya mchana, wawe na ujasiri wa kumkimbilia Bikira Maria, Mama wa Kanisa, ili awafundishe, kwani anawaelewa na atawasaidia.

“Kamwe vijana wasiridhike na mafanikio waliyopata, bali wawe na ujasiri wa kuthubutu kuota ndoto, kwa ajili ya ujenzi wa Ufalme wa Mungu sanjari na kuwasaidia walimwengu kujenga dunia inayofumbatwa katika udugu wa kibinadamu, ”amesema.

Amesema, ushuhuda wa imani uwawezeshe vijana, ili kwa kuona waweze kuamini. 

Kongamano hilo limehudhuriwa na Maaskofu wa Kanisa Katoliki, Mapadri, Watawa na Wana VIWAWA zaidi ya 3,000 kutoka majimbo  34 ya Kanisa Katoliki nchini, litamalizika Agosti 8,2022.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/98b1ee299e6fa003710ce9a63db3fe8c.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi