loader
Rais Samia ateua Majaji  22 wa Mahakama Kuu

Rais Samia ateua Majaji 22 wa Mahakama Kuu

RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa maofisa 22 akiwemo aliyekuwa Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata kuwa Majaji wa Mahakama Kuu kuanzia Agosti 4 mwaka huu.

Wengine ni Kelvin David Mhina aliyekuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, Adrian Philbert Kilimi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama, Happiness Philemon Ndesamburo, Kamana Stanley Kamana, Hamidu Rajabu Mwanga, Marlin Leonce Komba, Dk Mwajuma Kadilu Juma, Dk Cleophas K.K Morris na Asina Omari.

Pia walioteuliwa ni Aisha Zumo Bade, Mussa Kassim Pomo, Victoria Mlonganile Nongwa, Obadia Festo Bwegoge, Ruth Betwel Massam, Godfrey Ntemi Isaya na Gladys Nancy Barthy,.

Wengine ni Haji Suleiman Haji, Fatma Rashid Khalfan, Abubakar Mrisha, Lusungu Hemed Hongoli, na Monica Peter Otaru.

 


 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/68a264fdc7a1fd70f07500644290119e.jpeg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi