loader
Mtoto ajiua baada ya kugombezwa

Mtoto ajiua baada ya kugombezwa

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah amewataka wazazi kutafuta namna bora ya kuwaonya watoto wao wanapofanya makosa kuwaepusha wasichukue uamuzi mgumu ikiwemo kujiua.

Alitoa kauli hiyo baada ya mtoto wilayani Makete mkoani Njombe, kujiua hivi karibuni baada ya kugombezwa na mzazi wake kwa kuwaachia punda aliokuwa akiwachunga kula mazao kwenye shamba la mtu. Kamanda Issah alisema mtoto huyo alitumwa kuchunga punda lakini kutokana na michezo ya watoto, aliwaacha punda wakaenda kula mazao katika shamba la mtu.

Alisema mwenye shamba alikwenda kumlalamikia baba wa mtoto huyo kuwa punda wake wamekula mazao shambani kwake. Mzazi alimuita na kumfokea mwanaye na kumtaka awe makini anapokwenda kuwachunga punda. Kwa mujibu wa kamanda, kitendo hicho kilimkera mtoto huyo na kuchukua uamuzi wa kujiua kwa kunywa sumu.

“Wazazi wa Njombe na wazazi wa sehemu nyingine, likizo imewadia na imeshafika, tazameni namna ya kuzungumza na hawa watoto lakini watoto angalieni msiwe mmebadilika kiasi kwamba hata mzazi akikufokea kidogo tu unakasirika, msikasirike,” alisema Kamanda Issah na kuongeza: “Watoto wa sasa hivi tofauti na watoto wa zamani, fikiria unaweza ukamgombeza mtoto, mwingine akajinyonga, mwingine akafanya lolote ambalo siyo sawa sawa.”

Aidha, alisihi misikiti kupitia madrasa na makanisa kupitia shule za Jumapili kuwasaidia watoto kiroho wasifanye uamuzi wa ajabu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d4686eea4bc710ac9f0cc113c5b6dec0.jpeg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Na Matern Kayera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi