loader
Chalamila: Nimerudi mpya kuchapa kazi

Chalamila: Nimerudi mpya kuchapa kazi

MKUU wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amesema kuwa alikuwa likizo fupi kama gari bovu lililoharibika injini. Alisema hayo akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Meja Jenerali Charles Mbuge na kuongeza kuwa sasa amerudi kama gari jipya mjini kuchapa kazi.

Akizungumza na wakazi wa Mkoa wa Kagera na viongozi mbalimbali waliojitokeza kumpokea, alisema anahitaji ushirikiano wa dhati katika kuhakikisha anawaletea wananchi maendeleo na taifa kwa ujumla. Alisema ataanza kwa kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyotoa alipofanya ziara mkoani Kagera.

Aliwataka viongozi kuhakikisha wanatafuta njia ya kufanya Mkoa wa Kagera kuwa wenye uchumi wa juu kwa sababu una kila kigezo cha kuwa hivyo. Aliwataka wakuu wa wilaya kuondoa hofu ya kutoteuliwa badala yake wafanye kazi kwa bidii kwani vyeo vya kuteuliwa ni vya mzunguko na kila mmoja Mungu humpa kwa wakati wake.

Alisema kama watafanya kazi kwa hofu wakifikiria mkeka wa kuteuliwa tena kuendelea na nafasi zao, wananchi watakwama. Awali, Meja Jenerali Mbuge alimuomba mkuu Chalamila kufanikisha masuala ya kitaifa kwa kuanza na sensa ya watu na makazi, kufanikisha kuhitimisha mbio za mwenge kitaifa, kuhakikisha mradi wa bomba la mafuta unafanikiwa na wananchi wanalipwa fidia.

Mbuge aliwataka viongozi wote kushirikiana na mkuu huyo wa mkoa kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inafanikiwa na thamani ya fedha inaonekana. Alisisitiza kuwa lengo la serikali ni wananchi kupata huduma nzuri.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f06fbc8181035eb8a00902495807eeda.jpeg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Na Diana Deus, Bukoba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi