loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

25% waliofaulu Dar wakosa nafasi sekondari

Hayo yamesemwa jana na Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mapunda wakati wa kikao cha Kamati ya Uchaguzi wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wote wa Mkoa na Manispaa za Kinondoni, Ilala na Temeke.

Alisema matokeo mazuri ya ufaulu wa asilimia 76 ya Dar es Salaam na kuifanya kuongoza dhidi ya mikoa mingine nchini yamefanya viongozi wote wa mkoa huo kuwa na jukumu jingine la kuhakikisha wanafunzi hao wanapata shule ili kuwawezesha kuendelea na elimu yao ya sekondari.

Alisema kutokana na tatizo lililopo la ufinyu wa shule za sekondari pamoja na vyumba vya madarasa katika baadhi ya shule imekuwa vigumu wanafunzi wote waliofaulu kuchaguliwa huku vigezo vya ufaulu vilivyotokana na mwongozo wa Kamishna wa elimu kwa makatibu tawala wa mikoa ukizingatiwa ili kuwapata wanafunzi wenye sifa za kujiunga na shule mbalimbali.

“Uchaguzi huo wa wanafunzi hao umezingatia mwongozo wenye kumbukumbu No. CC.193/508/01/46 wa Oktoba 26 unaoelekeza kuwa wanafunzi wanaostahili kujiunga na kidato cha kwanza Mwaka 2014 kuwa ni wale waliofaulu kwa kupata alama kuanzia 100 hadi 250. “Kwa hatua hiyo wanafunzi 46,468 wakiwemo wavulana 22,562 na wasichana 24,086 walishindania nafasi za kuchaguliwa kwa usawa kwa kuzingatia ufaulu na machaguo pamoja na ukaribu wa shule ya sekondari husika” alisema Mapunda.

Alisema hatua hiyo ndiyo iliyosaidia kupata idadi hiyo ya wanafunzi 34,852 ambao ndiyo wataingia katika mchakato wa kuchaguliwa kujiunga na shule mbalimbali huku wanafunzi 10 wakichaguliwa kujiunga na Chuo cha Veta kama majaribio ya mara kwanza kwa uteuzi wa moja kwa moja.

Hata hivyo, alisema mpango ulikuwa kuwapa nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza wanafunzi wote waliofaulu isipokuwa uchache wa shule na ufinyu wa madarasa ndiyo kikwazo kilichosababisha wanafunzi wengine kukosa nafasi hiyo.

“Kuna shule zipo pembezoni mwa mji na zina nafasi, tatizo ni mazingira ambazo shule hizo zipo ikiwemo suala la umbali,” alisema Mapunda na kuongeza kuwa kama kuna mzazi ambaye mtoto wake kakosa nafasi lakini anaona anaweza kumudu gharama za kumpeleka mtoto wake katika shule hizo awasiliane na maofisa Elimu wa Manispaa apewe zitakazomuwezesha mwanawe kupata nafasi katika shule.

Alisema tatizo lililopo ni uhaba wa shule ambapo kati ya kata 90 kata 19 hazina shule za sekondari za wananchi jambo alilolitaka viongozi wa manispaa kujipanga na kuhakikisha wanaongeza vyumba zaidi vya madarasa.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi