loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

692 wanaswa wakiwinda Tarangire

Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Upendo Masawe alisema hayo wakati akitoa taarifa ya hifadhi hiyo kwa waandishi wa habari kutoka Chama cha waandishi wa habari mkoani Kigoma waliokifanya ziara katika hifadhi mbalimbali za taifa nchini na kusema kuwa majangili hao walikamatwa hifadhini hapo kuanzia mwaka 2003 hadi sasa.

Aidha Masawe alisema katika idadi hiyo jumla ya majangili 364 walikamatwa na nyara mbalimbali za hifadhi nje hifadhi ambapo watu 382 walikamatwa wakifanya ujangili ndani ya hifadhi.

Alisema hali hiyo imewalazimu kuongeza ulinzi na doria ndani ya hifadhi na katika maeneo ambayo yamekuwa mapito makubwa ya majangili wakati wanapoingia kufanya vitendo vya ujangili ndani ya hifadhi.

Pamoja na hilo, Mhifadhi huyo alisema wamekuwa wakitoa elimu kwa jamii ya vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo umuhimu wa kusaidia katika kulinda rasilimali za hifadhi na kutoa taarifa za uwepo wa vitendo vya ujangili.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Karatu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi