loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

900 wafaidika na huduma za umeme Mufindi

Jumla ya megawati nne zinazalishwa kupitia mradi wa umeme unaoendeshwa na Kampuni ya Rift Valley na kati yake, asilimia tano zimetengwa kwa ajili ya mahitaji ya wananchi huku zingine 95 zikiuzwa kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kupitia gridi ya Taifa.

Mradi huo unaozalishwa kwa maji, upo katika kijiji cha Isipii, kata ya Ihanu ambako ni zaidi ya Kilomita 160 kutoka makao makuu ya wilaya ya Mufindi, Mafinga mjini.

Meneja Uendeshaji wa mradi huo, Joel Gomba alisema kwamba mahitaji ya nishati hiyo kutoka kwa wananchi wa vijiji hivyo na vingine jirani vikiwemo vya wilaya ya Kilolo yanaongezeka siku hadi siku.

Alivataja vijiji vinavyonufaika na mradi huo kwa sasa ni pamoja na Isipii, Lulanda, Iyegela, Ibwanzi, Nandala, Ihanu, Kilosa, Ikanga, Kidete, Mlevelawa, Ikanin’gombe, Igoda, Luhunga na Mkonge.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Evarista Kalalu alisema kukamilika kwa mradi huo kumesaidia kwa kiasi kikubwa kuharakisha maendeleo ya wananchi wa vijiji hivyo na hivyo kuwapunguzia umasikini.

Mradi huo umejengwa kwa zaidi ya Sh bilioni 15.4 na kati yake asilimia 49.7 zilichangiwa na Jumuiya ya Ulaya (EU) na kiasi kilichobaki kilitolewa na mradi huo kupitia moja ya kampuni za Rift Valley, Kampuni ya Chai ya Mufindi (MTC).

MAFUNDI umeme nchini wametakiwa kufanya ...

foto
Mwandishi: Frank Leonard, Iringa

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi