loader
Picha

A. Mashariki yatakiwa kujali sanaa ya maigizo

Mwito huo ulitolewa jana na mchekeshaji maarufu wa Uganda, Anne Kansiime wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shoo yake anayoifanya leo kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam.

Alisema kupitia vichekesho, wananchi wanaweza kufikishiwa kwa urahisi ujumbe kuhusu amani na masuala mengine muhimu. Alisema sanaa hiyo ni rahisi kufikisha ujumbe ambapo wasanii wanatimiza azma yao hiyo huku wakiwa wanawafurahisha wananchi.

Alisema katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuna mengi ya kujadiliwa ambapo sanaa hiyo inawezafanya.

“Tanzania nimepapenda sana na hii ikiwa ni mara yangu ya kwanza kuja, nimependa sio tu nilivyopokelewa, bali hata inavyoonekana kuipenda sanaa hii na inatakiwa tuikuze kwa pamoja,” alisema mchekeshaji huyo maarufu.

Kwa upande wake, MC Pilipili mbali na kuwavunja mbavu waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo, lakini pia aliwataka wachekeshaji kutokwamishwa na lugha ya Kiingereza katika kutanua shughuli zao za sanaa hiyo kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki.

“Wachekeshaji wa hapa nchini zamani tulikuwa tukichukuliwa ni kama vile watu wa kawaida kabisa na tusiokuwa na maana, lakini kwa sasa tumefikia hatua ya watu kutukubali na tunatakiwa kujitambua na kujiendeleza,” alisema Mc Pilipili. Pia katika onesho hilo la leo, litahudhuriwa na mchekeshaji kutoka Kenya, Fred Omondi.

MABINGWA wa kihistoria Yanga leo wanashuka dimbani kuikabili Tanzania Prisons ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi