loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Afafanua ushuru magari yanayotoka Z'bar

Alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM).

Ole Sendeka alisema sera ya sasa ya magari yanayoingizwa nchini kupitia Zanzibar yanatozwa ushuru kidogo ukilinganisha na yale yanayopitia bara ambapo tofauti hiyo imekuwa chanzo kikuu cha kero ambayo Wazanzibar wanalalamika kuwa wanalipia ushuru mara mbili pale wanapoleta magari yao Tanzania Bara.

Mbunge huyo alitaka kujua lini Serikali itaweka ushuru unaolingana kwa pande zote mbili ili kuondoa malalamiko hayo. Akijibu swali hilo, Mkuya alisema Zanzibar bado wanatumia mfumo wa analojia, na wamekuwa wakifanya hivyo kutokana na Zanzibar uchumi wake kuwa mdogo.

Hata hivyo, Mbunge wa Mkanyageni, Habibu Mnyaa (CUF) alitaka kauli ya Serikali kwamba kero hiyo ya ushuru mara mbili itatatuliwa katika kipindi hiki cha uundwaji wa Katiba mpya baada ya kushindikana kwa takribani miaka 49.

Akijibu swali hilo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Samia Suluhu alisema kuna Tume kutoka pande zote za muungano ambayo inasimamia kero hiyo kwa sasa.

Alisema tume hiyo inatarajia kuleta taarifa yake serikalini na baadaye Serikali itatoa mwelekeo wa nini kifanyike. Katika swali la msingi, Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji (CUF), alitaka kujua utaratibu gani unatakiwa kutumika pale Watanzania kutoka Zanzibar wanapotaka kuingia Tanzania bara na magari yao kwa lengo ya kuyatumia kwa muda maalum.

Akijibu swali hilo, Mkuya alisema utaratibu unaotumika hivi sasa ni kuruhusu magari yaliyoandikishwa Zanzibar kutumika bila kuandikishwa Tanzania bara kwa muda wa miezi mitatu.

Alisema Naibu Kamishna wa Ushuru na Forodha Zanzibar hulitambulisha gari linalokuja Tanzania Bara kwa muda na sababu maalumu kwa Kamishna wa Ushuru na Forodha Tanzania Bara ambaye ataruhusu gari husika.

Mkuya alisema utaratibu huo hutumika kwa magari yote yanayotoka nje ya nchi kuingia Tanzania Bara.

RAIS John Magufuli amesema Manispaa ya Ilala imepandishwa ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi