loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Afrika Kusini, Tanzania kuimarisha uhusiano wa kibiashara

Juhudi za karibuni kuimarisha uhusiano huo, zimeshuhudiwa wiki hii ambapo wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka nchi hiyo kubwa kiuchumi Afrika walitembelea nchini kwa mazungumzo zaidi.

Ujumbe huo ulihudhuria semina kuhusu biashara kati ya nchi hizo iliyofanyika juzi jijini Dar es Salaam, ambayo ilitayarishwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya semina hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Juliet Kairuki, alisema mazungumzo yao yalilenga kuangalia namna nchi hizo zitakavyofaidika kwa kuboresha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji.

Wawekezaji hao kutoka Afrika Kusini, wameonesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya kilimo na kuchagua mikoa ya Mwanza na Morogoro kama maeneo ambayo wangependa kuwekeza.

Semina ya biashara ya wiki hii ni matunda ya Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa lililofanyika mkoani Mwanza Februari mwaka huu.

Baada ya kongamano hilo, Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini, Thanduyise Chilliza ambaye alichukua hatua na kuwa mjumbe wa kutangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana Tanzania kwa wawekezaji katika nchi yake.

Kairuki alisema kwa kushirikiana na Afrika Kusini, Tanzania itafaidika na teknolojia mpya, masoko, uongozi na usimamizi wa miradi mikubwa ya kilimo miongoni mwa faida nyingine.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera alisema amejifunza mengi katika semina hiyo.

“Tumejifunza mengi kutoka kwa hawa wenzetu wa Afrika Kusini hasa katika masuala ya kilimo cha mboga na viungo,” alisema Mkuu wa Mkoa.

Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya, alisifu semina hiyo na kusema TIC imefanya kazi nzuri. “Semina hii imetufungua macho katika mambo mbalimbali,” alisema.

Meneja Mtendaji, Export Development and Promotion, Trade and Investment KwaZulu Natal, Lester Bouah alisema ni kwa kushirikiana pamoja ndipo fursa zitapatikana na maendeleo ya kweli kufikiwa.

KAMPUNI ya uchimbaji ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi