loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Afya wajivuna kufika lengo la Milenia kwa watoto

Waziri Seif ameyasema hayo jana mjini Moshi, wakati akifungua mafunzo ya wasimamizi na wadadisi wa utafiti wa tathimini ya utoaji wa huduma za afya nchini (TSPA) katika ukumbi wa Uhuru Hosteli mkoani Kilimanjaro.

Alisema matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 anaonesha vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano vimepungua kutoka vifo 81 kwa kila watoto waliozaliwa hai 1,000 mwaka 2000 na kufikia vifo 66.5 kwa watoto waliozaliwa hai 1,000 mwaka 2012.

Dk Seif alisema pia serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya watoto na vifo vya akinamama vinavyotokana na uzazi.

Alisema takwimu zinaonesha kuwa vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka 51 kati ya watoto waliozaliwa hai 1,000 kwa mwaka 2010 na kufikia vifo 45 kati ya watoto 1,000 waliozaliwa hai.

“Taarifa hii inaonesha juhudi za serikali zimeiwezesha Tanzania kufikia Malengo la Milenia la kupunguza vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano kwa theluthi mbili...hivyo nawaombeni muweke uzalendo mbele kwa ajili ya kutafuta takwimu za uhakika na sahihi kwa maendeleo ya taifa,” alisema Dk Seif.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk Albina Chuwa alisema mafunzo hayo yamejumuisha wauguzi wawili kutoka kila mkoa, ambapo yatakuwa na lengo la kuwafundisha jinsi ya kukusanya takwimu zinazohusu Utafiti wa Tathimini ya utoaji wa huduma za afya kwa mwaka 2014/2015.

Alisema mafunzo hayo yatawawezesha kutambua namna gani vituo vya afya vilivyojipanga katika kutoa huduma bora za afya, kwa kuangalia upatikanaji wa huduma mbalimbali, vifaa, miundombinu pamoja na rasilimali watu.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Arnold Swai, Moshi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi