loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Aggreko yazindua mitambo kufua umeme

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, baada ya kuzindua kituo hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Aggreko, Kanda ya Afrika Mashariki, David Edwards, alisema uzinduzi huo umelenga kusogeza huduma karibu zaidi kwa Watanzania na kuwaondolea usumbufu wa uagizaji wa mitambo hiyo kutoka nje ya nchi.

Alisema kimsingi kampuni hiyo imekuwa ikifanya kazi ya kutoa huduma ya nishati mbadala kwa zaidi ya miaka 15 katika nchi mbalimbali Afrika, ikilenga kukabiliana na changamoto zote za nishati zinazojitokeza maeneo, mbalimbali ikiwemo viwandani, migodini na kwingineko.

“Katika miaka hiyo 15 ndani ya Bara la Afrika tumefanya kazi katika miradi mikubwa ukiwemo wa usambazaji wa Megawati 240 za umeme nchini Kenya, Megawati 40 katika mradi wa gesi Tanzania huku tukiajiri wafanyakazi 6,000 katika maeneo 202 tuliyopo katika nchi 100 duniani kote,” alisema.

Alisema uzinduzi wa kituo cha Aggreko kilichopo eneo la Mwenge Dar es Salaam ni mkakati wa muda mrefu wa kampuni hiyo kwa Tanzania kutokana na fursa nyingi za kiuchumi zilizopo zinazovutia wawekezaji wengi kuja na kuwekeza katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya viwandani na migodini.

Aidha, alisema uchumi wa Tanzania umeanza kuonesha dalili njema za kukua kwa kasi kutokana na uchimbaji wa gesi asilia unaotarajiwa kuanza kufanywa hivi karibuni katika mikoa ya kusini na kusisitiza una faida kubwa kwa kuwa mbali na mambo mengine kwa kiasi kikubwa utasaidia kupunguza tatizo la nishati ya umeme hapa nchini.

Pia alisema mbali na hapa Tanzania, kampuni hiyo imefanya kazi katika nchi za Afrika Kusini, Ethiopia, UK, Ufaransa, Ivory Coast, Msumbiji, Indonesia, Bangladesh, Argentina, Venezuela, Chile, Brazil na Marekani.

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania imetangaza ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi