loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ahimiza viongozi wa dini kuombea Taifa

Kauli hiyo imetolewa wakati wa kisomo cha sherehe ya Maulid zilizofanyika katika msikiti wa Munawwarat, Mtoni Kijichi, Dar es Salaam na Mhasibu Mkuu wa Mkoa huo, Shabani Mhando wakati akizungumza na wamumini na viongozi wa dini ya Kiislamu waliohudhuria sherehe hiyo.

Akizungumzia kuhusu suala la amani alisema, viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuiondolea serikali na vyombo vya dola ulazima wa kuwakamata vijana na kuwafungulia mashitaka kutokana na kufanya vurugu na vitendo vya uvunjaji wa amani.

“Mwaka huu hadi kufikia Oktoba kuna mambo matatu makubwa, kwanza ni kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, kura ya maoni ya katiba mpya na uchaguzi mkuu, katika masuala haya muhimu ni vema bila kujadili itikadi za kidini, siasa au kabila tujipange katika kushiriki kikamilifu,” alisema Mhando.

Alisema sherehe hiyo ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad ‘Swallah Llahu Alayhi wa Sallam’, zina maana kubwa kwa waislamu na jamii yote kwa ujumla, kutokana na kuwa mtume ni nuru, mwokozi na mwenye huruma kwa umma na ndiyo sababu ya kuwepo kwa amani katika umma huu na hilo limethibitishwa katika Kurani.

WACHIMBAJI wa mchanga wamebanwa kutokana ...

foto
Mwandishi: Katuma Masamba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi