loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ajali yaua 3, kujeruhi 46

Ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili T 680 ARL mali ya Ngassa Seni mkazi wa Kiloleli wilayani humo, lililokuwa likiendeshwa na dereva Shija Ngassa.

Gari hiyo lilikuwa likienda kwenye mnada wa Mhunze katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na lilipinduka baada ya kuacha njia.

Mmoja wa majeruhi hao Kashindye Mkaa alisema gari hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi na walipofika kwenye kona liliacha njia na kupoteza mwelekeo kisha kupinduka.

Hata hivyo, Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga, Daniel Maguja alikiri kupokea majeruhi hao huku akisema kuwa watu wawili walikufa wakiwa wanapelekwa hospitali na watatu alikufa akiwa hospitalini hapo akipatiwa matibabu.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa, Justus Kamugisha alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa imetokea saa 3:00 asubuhi katika kijiji cha Uchunga ambapo chanzo chake kimeelezwa kuwa ni mwendo kasi.

CHAMA cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) kimekubaliwa ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy, Shinyanga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi