loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Akana kumng'ata 'housegirl' wake

Alisomewa maelezo hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mbele ya Hakimu Yohana Yongolo.

Wakili wa Serikali Tumaini Msikwa alidai kati ya Januari na Juni mwaka huu, maeneo ya Mwananyamala Wilaya ya Kinondoni, Maige alimng’ata Yusta Kashinde(20) sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu.

Mshitakiwa alikana maelezo aliyosomewa na kwamba aliiomba mahakama kumpatia dhamana.

Wakili Msikwa aliiambia mahakama kuwa dhamana ya mshitakiwa imezuiliwa kama awali kwa kuwa bado wananchi wana hasira hivyo kuhofia usalama wake. Hakimu Yongolo alisema shauri hilo litaanza kusikilizwa Julai 10 mwaka huu.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi