loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Aliyeingia fainali Madola awa wa 8

Hayo yalielezwa na Meneja wa timu hiyo ya Tanzania iliyoshiriki michezo hiyo iliyomalizika jana Glasgow, Scotland huku mwanariadha wake wa mita 1,500, Bazil Baynit akishindwa kupata medali.

Baynit aliyekuwa tegemeo pekee lililobaki katika riadha baada ya wenzake kuchemsha, alimaliza fainali ya mbio hizo akiwa wanane kwa kutumia muda wa dakika 3:41.74 huku mshindi wa mbio hizo akiwa Mkenya James Magut aliyetumia 3:39.31.

Akizungumza kwa simu kutoka Glasgow, meneja wa timu hiyo, Muharami Mchume alisema wasiwasi wa mashindano kuwa ni moja ya sababu zilizochangia kufanya vibaya kwa wachezaji katika michezo hiyo.

Mchume alisema inaonekana kama kuna wasiwasi fulani kila mchezaji wa Tanzania anapoingia katika mashindano licha ya kuanza vizuri, lakini muda unapozidi kwenda ndio anazidi kuvurunda.

Alisema hiyo huenda inasababishwa na kutokuwa na uzoefu wa kushiriki mashindano ya kimataifa mara kwa mara, ambayo yangewaondolea woga na mashindano kuyaona ya kawaida, tofauti na sasa.

“Inaelekea wachezaji wetu kila wanapoingia kushindana huwa na wasiwasi wa mashindano na hiyo ndio nafikiri sababu kubwa ya wao kushindwa licha ya baadhi yao kuanza vizuri," alisema Mchume na kuongeza:

“Na sio kama hawaanzi vizuri, utakuta mtu ananza vizuri lakini mchezo unapoelekea mbele ndio anapoteza mwelekeo na huwa kama wanaogopa mashabiki wengi waliojazana uwanjani, hawajazoea.”

Mchume alitolea mfano wachezaji wa mpira wa meza ambao alisema sio kama walikuwa hawashindi, walianza kwa ushindi, lakini baadaye unakuta wenyewe (Watanzania) ndio wanakuja kupoteza mchezo huo.

Akiongeza kwa kutolea mfano timu ya kunyanyua vitu vizito, alisema mchezaji alipokuwa nchini, alikuwa akibeba hadi kilo 105, “lakini alipofika kwenye mashindano mbele za mashabiki anashindwa kubeba kilo hizo.”

Mbali na riadha, Tanzania pia ilipeleka michezo ya ngumi, kuogelea, kunyanyua vitu vizito, mpira wa meza na judo, ambazo hazikufua dafu.

Klabu ya Liverpool na Manchester United zipo vitani kumuwinda ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi