loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Amani iwe jadi yetu, tuilinde

Wengi wetu tumejaaliwa kwa neema za Mungu, kufika siku hii ingawaje wapo wenzetu wachache, ambao inawezekana wamepatwa na masaibu mbalimbali na kushindwa kushiriki kikamilifu kufunga na hatimaye kushiriki sherehe zenyewe za Idd el Fitr.

Hapa tunapenda kuungana na mawaidha, yaliyotolewa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal katika salama za Idd el Fitri katika ibada ya kitaifa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, ambapo aliwataka Watanzania kwa umoja wao, kulinda amani kwa uwezo wao wote.

Dk Bilal alisema watu wote, bila kujali dini zetu, tuimarishe upendo, amani na ushirikiano baina ya watu na watu na pia baina ya dini zetu mbalimbali na sio kwa Waislamu pekee.

Viongozi wetu wengi wa dini na serikali, waliungana pia na Makamu wa Rais katika kutoa mwito mwema, unaoshabihiana na huo ili kwa pamoja kama Taifa, tuendelee kuwa kisiwa cha amani na upendo.

Katika hili, Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum aliweka bayana kwa kusisitiza umuhimu wa amani, kwamba dini ya Kiislamu sio dini ya kigaidi, hivyo iwapo Muislamu anapopatikana na hatia ya ugaidi, ahukumiwe yeye binafsi na sio dini yake.

Alitoa mfano wa mabomu, yaliyolipuliwa katika maeneo kadhaa nchini kwa siku za hivi karibuni, kuwa siyo Uislamu huo kwani dini ya Kiislamu hairuhusu kufanya mambo kama hayo na hivyo kushauri mtu wa aina hii, ahukumiwe kama mtu binafsi. Tunapenda kukumbushana katika suala hili la amani, kwamba ni vizuri kila mmoja wetu awe mlinzi wa mwenzake.

Hapa tunamaanisha kwamba yeyote kati yetu anayepanga kutuvuruga Watanzania, kwa kisingizio chochote kile, ikiwa ni pamoja na kututenga kwa mithili ya dini, ukabila, itikadi na rangi asivumiliwe, bali afichuliwe ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake.

Hivi inakukera nini kuona viumbe wa Mungu, wanaishi kwa amani na utulivu na kushirikiana katika shida na raha? Labda, pia tujiulize kwa wenzetu wanaopenda tufarakane, watapata nini kwa kuleta vurugu katika jamii.

Ni kutokana na hoja hizo, basi ndiyo maana tunasema kila mmoja wetu, awe makini na yeyote ambaye hatutakii mema watanzania. Tukishirikiana na kushikamana, maadui zetu hawatapata mwanya huo wanaoutafuta.

Letu kubwa hivi sasa ni kuongeza bidii katika vita dhidi ya ujinga, maradhi na umasikini ili kujiletea maendeleo endelevu, jambo ambalo sisi tunaamini linawezekana.

Sisi ambao tumekuwa kwa muda mrefu kimbilio la wenzetu kutoka nchi mbalimbali ili kupata amani, tusiwe wa watu wa kukaribisha vurugu, bali kuilinda amani yetu idumu daima.

RIPOTI ya 15 kuhusu uchumi wa Tanzania ya ...

foto
Mwandishi: mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi