loader
Dstv Habarileo  Mobile
Amina Ngaluma ‘Japanese’ afariki dunia

Amina Ngaluma ‘Japanese’ afariki dunia

Ngaluma amefariki dunia jana nchini Thailand ambako kwa kushirikiana na Watanzania wenzake, wanaendesha shughuli za muziki.

Kwa mujibu wa mdogo wake, Abdallah Ngaluma, dada yake amefariki dunia kutokana na shinikizo la damu baada ya kuwa amelazwa tangu Jumapili iliyopita, baada ya kupatwa na ugonjwa huo.

“Ni kweli dada Amina Ngaluma amefariki dunia leo (jana) nchini Thailand ambako anafanya kazi zake kwa muda sasa. Msiba upo nyumbani kwa wazazi wetu Kitunda Machimbo, Dar es Salaam,” alisema Abdal lah jana.

Ngaluma aliyekuwa na sauti nyororo na anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 41, amekuwa akifanya kazi za muziki nchini Thailand tangu mwaka 2011, lakini alirejea nchini Juni mwaka jana na kukaa kwa muda mfupi kabla ya kurejea katika nchi hiyo ya Asia.

Kabla ya kwenda huko, kuanzia mwaka 2007 alikuwa akienda Dubai na nchi nyingine za Uarabuni, kufanya kazi za muziki na kurejea nchini baada ya kuwa ameachana na Bendi ya TOT Plus.

Ngaluma aliwika na kutamba akiwa na Twanga Pepeta katika bendi yake ya African Revolution ‘Tamtam’ ambako akiwa na Mwinjuma Muumini na Badi Bakule, walitamba na wimbo wa Mgumba.

Mbali ya wimbo huo wa Mgumba, Ngaluma ‘Japanese’ alitunga nyimbo mbili za Mapendo na Manyanyaso Kazini, kabla ya kuhamia Double M Sound ambako aliachia wimbo wa Poleni Wajane.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi