loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Amref kusaidia kupunguza vifo vya wajawazito

Watapatiwa mafunzo kupitia kampeni yake ya kupunguza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua.

Kutokana na hali hiyo, shirika hilo limepanga kuongeza nguvu na juhudi za kutunisha mfuko wa kimataifa wa kusaidia mafunzo hayo kupitia kampeni iitwayo Stand Up For African Mothers.

Mkurugenzi Mkazi wa Amref Tanzania, Dk Festus Ilako, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana. Alisema Oktoba 9 mwaka huu katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam watafanya harambee kwa ajili ya kukusanya fedha kusaidia kampeni hiyo.

“Kwa kuamini kuwa hakuna mwanamke anayepaswa kufa wakati wa kujifungua, Shirika la Amref Health Africa Tanzania kwa kushirikiana na Bank M na Barclays zinatangaza nia ya kuongeza nguvu na juhudi za kutunisha mfuko wa kusaidia mafunzo ya wakunga kupitia kampeni yake ya Stand Up for African Mothers,” alisema.

Alieleza kuwa kampeni hiyo ya kimataifa, inalenga katika kuongeza uelewa juu ya mchango unaotolewa na wakunga wenye ujuzi katika kupunguza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua.

“Kampeni hii pia inalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wakunga 15,000 katika nchi 13 za Afrika, kati yao wakunga 3,800 wanatarajiwa kupata mafunzo nchini Tanzania ifikapo mwaka 2015/2016. Kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘Changia Mafunzo ya Wakunga, Okoa Maisha ya Mtoto’,” alisema.

Alisema kwa Tanzania kampeni hiyo ilizinduliwa na Mke wa Rais, Salma Kikwete Mei 15 mwaka 2012, ambapo Mama Salma amekuwa balozi mzuri wa kampeni hiyo.

Naibu Mkurugenzi wa Amref Tanzania, Dk Ritha Norowha, alisema fedha zilizopatikana mwaka jana zitasaidia wanafunzi 60 watakaoanza masomo mwezi ujao.

WASHEREHESHAJI katika matukio mbalimbali zikiwamo sherehe za harusi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi