loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Angetile afutwa kazi TFF

Angetile, ambaye amekuwa katika wadhifa huo tangu Desemba 2011, ameagizwa aende likizo ya malipo hadi mkataba wake utakapomalizika, hivyo TFF kujiandaa kupata Katibu Mkuu mpya.

Kwa mujibu wa aliyekuwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga, wakati akikabidhi ofisi juzi kwa Malinzi, waajiriwa wa shirikisho hilo ambao ni Katibu Mkuu na wakurugenzi, wapo katika kipindi cha nyongeza cha miezi sita cha mikataba yao kinachoishia mwishoni mwa Desemba mwaka huu, 2013.

Lakini jana, Rais wa TFF, Malinzi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Dar es Salaam, alisema: “Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF. Uteuzi huo ni kuanzia Novemba 2 mwaka huu.“Aidha, aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameagizwa aende likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake.” “Kamati ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Bwana Boniface Wambura katika utekelezaji wa majukumu yake,” aliongeza Malinzi ambaye Kamati yake ya Utendaji ilikutana kwa mara ya kwanza juzi Jumamosi.

Wambura kitaaluma ni mwandishi wa habari na mwanasheria na alijiunga na TFF, pamoja na Angetile, Desemba 2011 baada ya kuondoka kwa Florian Kaijage na Frederick Mwakalebela.

Akizungumza na gazeti dada na hili, SpotiLeo jana, Angetile ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, alisema atatoa taarifa kwa vyombo vya habari leo.

Akizungumzia uamuzi huo wa Kamati ya Utendaji ya TFF, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Michael Wambura alisema hiyo ni taratibu ya kawaida katika ajira, hasa kwa kuwa mhusika alikuwa amebakiza miezi michache amalize mkataba wake.

“Hili ni suala la kawaida katika ajira. Hata mfanyakazi anapokaribia kustaafu anapelekwa likizo. Na huyo atakuwa likizo, tena ya malipo. Lakini pia mkataba wake ulikwisha, akaongezewa muda. Lakini zaidi kuna regime (utawala) mpya ambao umeingia pale,” alisema Wambura na kuongeza: “Kwa hiyo si kwa Angetile tu, na hata wakurugenzi wengine, walipaswa ama kuandika barua za kujiondoa au kusubiri uongozi mpya ufanye maamuzi. Walipaswa kusoma alama za nyakati.”

Mbali na Katibu Mkuu Angetile, wakurugenzi wa TFF ni Sunday Kayuni (Ufundi), Saad Kawembwa (Mashindano) na Jimmy Kabwe (Masoko).

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi