loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Arusha wapaisha ufaulu darasa la 7

Aidha halmashauri na wilaya za mkoa huo zimeaswa kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara zinazoendelea kujengwa ili kuweka vizuri mazingira ya kusoma kwa wanafunzi.

Hayo yalisemwa jana jijini hapa na Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Arusha, Anza Ndossa kwenye ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Uchaguzi wa Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2014.

Alisema matokeo ya ufaulu kwa mwaka huu ni sawa na asilimia 58.66 ambapo wanafunzi waliofanya mtihani mwaka 2013 walikuwa ni 35,344 na wavulana walikuwa 16,894 huku wasichana wakiwa 18,450.

Alisema waliofaulu ni 20,733 kati yao wavulana walikuwa 9,869 na wasichana 10,864 na kuongeza kuwa matokeo ya mwaka huu yalikuwa na lengo la ufaulu kwa asilimia 60 na malengo ya kitaifa chini ya mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika sekta ya elimu.

“Kimkoa tupo nyuma ya malengo ya BRN kwa asilimia 1.33 lakini tunatarajia mwakani lengo letu litakuwa ni asilimia 70 ingawa kuna baadhi ya halmashauri zimefanya vizuri lakini tujitahidi kuhakikisha tunakutana na wazazi/ walezi ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi’’.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi