loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Askofu aonya wanasiasa

Akizungumza jana jijini Dar kuhusu kongamano la Uponyaji wa Nchi kwa ajili ya kuombea nchi katika kuelekea kipindi cha uchaguzi, Komanya alisema mtu yeyote anayetaka kuwania nafasi za uongozi anatakiwa kumtanguliza Mungu.

“ Uchaguzi huu tumeamua kuweka (madarakani) wanaostahili, mbunge atakayeshirikiana na waganga wa kienyeji hatapenya, kwa sababu tuna maagano na nchi kwa sasa. Natoa tamko kama nabii, mbunge ukipita kwa staili ya waganga, baada ya kuapishwa, mwezi mmoja hauishi hutakaa jimboni kwako safari zako zitakuwa ni za mahangaiko ya magonjwa,” alisema.

Alisema badala ya wabunge kupeleka fedha kwa waganga wa kienyeji wanatakiwa kuzitumia katika kusaidia wahitaji, wakiwamo yatima na wajane.

Kuhusu sifa za rais ambaye anafaa kuchaguliwa, Komanya alisema anatakiwa mtu mwenye msimamo, asiyeyumbishwa na mwenye uamuzi mgumu, sifa ambazo pia zinatakiwa kwa viongozi wengine wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi.

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi