loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

'Askofu muwe na hofu ya Mungu'

Pia wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kufuata misingi ya dini na kwamba viongozi wengi wanapokuwa kwenye madaraka wanasahau kuwa wao ni miongoni mwa waumini wa dini ambao siku moja watahukumiwa kwa matendo waliyoyafanya wakiwa hapa duniani.

Akiwahutubia maelfu ya wananchi na viongozi wa serikali wakati wa ibada ya misa takatifu ya kuuombea mwili wa Meja Jenerali mstaafu Rowland Makunda, Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Masasi, James Almasi alisema viongozi wengi wamekuwa wakifanya baadhi ya maamuzi kwa maslahi yao binafsi kana kwamba wao ni miungu watu.

Alisema wananchi wamechoshwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wao ambapo kwa sasa nchi ya Tanzania inahitaji viongozi wenye kiu ya kumuona Mungu na wale wenye hofu ya Mungu na kwamba viongozi wa dini zote hapa nchini wamekuwa wakitoa malalamiko yao kila mara lakini cha ajabu wamekuwa wakiambiwa kuwa wao ni miongoni mwa wafuasi wa Ukawa.

Kwa mujibu wa Almasi, maisha aliyoishi Makunda yanapaswa kuigwa na kila kiongozi wa nchi kwa nafasi yake, kwani ni viongozi wachache wenye madaraka wanaoweza kuishi maisha ya kumtumaini Mungu kama Makunda.

Alisema wakati wa uhai wake mara baada ya kustaafu Jeshi Meja Makunda alishirikiana na wananchi wa kawaida bila kujali wadhifa wake, alikuwa ni mtu mwenye huruma, hofu ya Mungu na aliyependa kutoa msaada kwa kila mtu mwenye shida na katika kudhihirisha hilo kila siku ya Ijumaa alikuwa anatoa msaada kwa watu wenye ulemavu pamoja na wazee nyumbani kwake.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Clarence Chilumba, Masasi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi