loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ataka elimu dhidi ya ukatili kuimarishwa

Mgeni alisema hayo wakati akiyafungua maonesho ya asasi za kiraia katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya mji wa Unguja ambayo yamezijumuisha jumla ya asasi 80 zikiwemo za Tanzania Bara.

Alisema mchango wa asasi hizo katika kutoa elimu ya masuala mbalimbali ni mkubwa na ndiyo maana Baraza la Wawakilishi linafanya kazi zake bega kwa bega na asasi hizo.

Alisema wakati umefika kwa asasi hizo kutoa Elimu ya uraia kuhusu masuala ya uchaguzi ili kupata ushiriki kamili wa wananchi katika masuala ya siasa.

Alisema katika siku za hivi karibuni kumejitokeza tabia ya wananchi kukosa ushiriki mzuri wa masuala ya kisiasa pamoja na kushiriki katika uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Asasi za kiraia( Angoza) Zanzibar, Asha Aboud alisema wakati umefika Serikali kuzifanyia kazi sheria ambazo zinaonekana hazifanyi kazi pamoja na kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo na kiuchumi.

Alisema mchango wa asasi za kiraia ni mkubwa katika kuleta mabadiliko ya maendeleo katika jamii na uchumi. Kwa mfano alisema wakati umefika kwa Serikali kuifanyia marekebisho haraka sheria ya Serikali za mitaa ambayo lengo lake kuwashirikisha wananchi katika kuleta maendeleo.

“Tunawaomba wajumbe wa Baraza la Wawakilishi tushirikiane katika kuleta maendeleo katika kuwashirikisha wananchi kuleta mabadiliko ya sheria,”alisema.

Baadhi ya Wawakilishi walioshiriki katika maenesho hayo ya kazi za Asasi za Kiraia, Mahmoud Thabit Kombo alisema Asasi za Kiraia zinatakiwa kufanya kazi kubwa katika kuleta mabadiliko ya jamii.

Kwa zaidi ya miaka mitano sasa asasi za kiraia zimekuwa zikifanya maonesho kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ambao ndiyo wawakilishi wa wananchi.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi