loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Atuhumiwa kumuua mkewe kwa wivu

Mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akifanyakazi ya kusimamia shamba na kuendesha bodaboda, anatuhumiwa kufanya mauaji hayo nyumbani kwa wakwe zake baada ya kukataliwa na mkewe huyo katika kikao cha usuluhishi wa ugomvi kati yao.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa Kijiji cha Boko nyumbani kwa mwanamke huyo, Mnemela Mohamed alisema kuwa tukio hilo lilitokea Julai 27 majira ya saa mbili asubuhi.

Mohamed alisema kuwa siku moja kabla ya tukio hilo yaani Julai 26 mtuhumiwa huyo akisindikizwa na rafiki yake mmoja ambaye jina lake halikupatikana, walikuwa na kikao cha kusuluhishwa baada ya kuhitilafiana na mkewe ambacho kilifanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu.

“Kwa mujibu wa watu waliohudhuria, kikao hicho kilifanyika kuanzia majira ya saa 2 usiku hadi saa 5 usiku ambapo mwafaka haukuweza kufikiwa kwani marehemu alikataa kwenda kwa mume wake,” alisema Mohamed.

Alisema siku iliyofuata, watu waliokuwa wakihusika kusuluhisha waliondoka wakiwa pamoja na huyo mtuhumiwa na rafiki yake, lakini ghafla alirudi akidai kuwa anafuata betri ya simu aliyoisahau nyumbani kwao na marehemu.

“Alimkuta mkewe akipepeta mchele jikoni na kuanza kumbembeleza lakini aligoma kabisa kurudi kwa mumewe, hali iliyomkasirisha mumewe na kuanza kumchoma kwa kutumia kisu huko huko jikoni, kisha wakatoana nje huku marehemu akipiga kelele kuomba msaada,” alisema Mohamed.

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi