loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Aveva ataja vipaumbele Simba

Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika juzi kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay, Aveva ambaye ni mmoja wa wanachama wanaounda kundi la ‘vibopa’ la Friends of Simba, alichaguliwa kuwa Rais baada ya kupata kura 1,460 dhidi ya kura 378 za mpinzani wake pekee, Andrew Tupa.

Katika nafasi ya Makamu wa Rais, aliyeshinda ni Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ aliyepata kura 1,406 na kuwashinda Sued Mkwabi aliyepata kura 373 na Jamhuri Kihwelu Julio 412.

Katika nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji, waliopata nafasi hiyo ni Jasmini Sudi aliyepata kura 933, Ali Suru 627, Said Tully 788, Iddy Kajuna 893, Collin Fish 794.

Walioshindwa na kura zao katika mabano ni Amina Poyo (330), Asha Muhaji (623), Ally Chaurembo (229), Juma Mussa (51), Abduhamid Mshangama (540), Chano Almasi (232), Yassin Mnete (189), Ibrahim Masoud (358), Said Kubenea (615), Hamis Mkoma (205), Rodrin Chiduo (621), Said Pamba (220), Idd Mkambala (152) na Danny Manembe (138).

Akizungumzia ushindi wake, Aveva alisema ni ushindi mkubwa na wenye mafanikio kwa maendeleo ya klabu pamoja na soko zima la soka kwa ujumla wake.

Aveva ambaye anachukua mikoba ya Ismail Aden Rage ambaye hakuwania kiti hicho, alisema kuchaguliwa kwake huko ni mwanzo wa mafanikio ya kweli katika kuifikisha klabu hiyo kwenye ngazi za kimataifa pia.

“Mimi kwa sasa ninachoomba wanachama wote wa Simba kuzika tofauti zetu, kuhakikisha kuwa tunaiendeleza Simba na kuepuka kila aina ya mpasuko kujitokeza,” alisema Aveva na kuongeza:

“Katika uchaguzi kulikuwa na mengi yaliyojitokeza kama vile wanachama kugawanyika katika kupigania ushindi wa mgombea waliokuwa wakimtaka na hiyo ni hali ya kawaida katika kila uchaguzi.”

Alisema kwa sasa ni kujipanga vema zaidi na Kamati yake ya Utendaji na kitachobakia itakuwa ni kuhakikisha kuwa wanapigania mafanikio zaidi. Kwa upande wake, Jasmine alisema anajisikia furaha kuchaguliwa kuwakilisha katika nafasi ya wanawake.

Alisema wanawake ni kiungo kikubwa kwenye mafanikio ya klabu na atahakikisha kuwa mchango wao unaonekana kwenye klabu hiyo kwa kuwa umuhimu wao ni zaidi ya kuishia kushangilia timu tu.

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais mpya, Geoffrey Nyange ‘Kaburu,’ amesema wakati wowote kuanzia leo watakutana ili kuweka mikakati yao ya kuiandaa timu kwa ajili ya kufanya vizuri msimu ujao. Kaburu alisema wanakusudia kufanya kazi kama timu kama walivyoahidi kwenye kampeni zao.

“Nawashukuru wanachama wa Simba kwa kunipa nafasi ya kuwa Makamu wa Rais, yale yote niliyoyaahidi nitayatekeleza kama nilivyosema wakati tunapita kwenye matawi mbalimbali,” alisema Kaburu.

Alisema watakutana na kuzungumza mikakati yao, lakini pia timu inatarajia kuanza maandalizi kwa ajili ya Ligi Kuu msimu ujao, hivyo, baada ya kikao chao wataweka bayana waliosajiliwa ni wapi.

Awali, alisema wamesajili wachezaji wawili wakali, pia, kwamba wanatarajia kuvunja mikataba na baadhi ya wachezaji walio waona katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Alisema msimu huu, Simba ifanye vizuri kwa vile wale wote marafiki wa Simba ambao waliahidi kufanya usajili mzuri wamepita, hivyo, wana wajibu wa kutimiza kile walichokiahidi.

“Naamini kwa pamoja tutashinda, tunataka kutengeneza timu yenye ushindani wa kweli, hilo tumedhamiria, lengo letu ni kuongeza ustawi wa soka katika klabu yetu,” alisema Kaburu aliyekuwa Makamu Mwenyekiti chini ya Rage kabla ya kujiuzulu.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi