loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Aveva Rais mpya Simba

Kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi, Aveva alikuwa amepata kura takriban 1,456 dhidi ya kura 378 za mgombea mwenzake.

Katika nafasi ya Makamu wa Rais aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ameshinda wadhifa akiwapiku wagombea wengine, Sued Mkwabi, Jamhuri Kihwelo na Bundala Kabulwa.

Awali, Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Klabu ya Simba ulifanyika jana huku ukigubikwa na mizengwe ya aina mbalimbali. Wanachama zaidi ya 2,000 walijitokeza kwenye uchaguzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo wa uchaguzi huo, mgombea aliyeenguliwa kugombea nafasi ya Rais Wambura alizuiliwa kuingia kwenye ukumbi huo. Wambura aliwasili katika eneo hilo mapema tayari kwa kuudhuria Mkutano Mkuu ambao ulifuatiwa na uchaguzi, lakini aliambiwa kuwa jina lake halipo kwenye orodha ya wanaotakiwa kuingia.

Kutokana na hali hiyo, alikaa nje kwa muda na kisha kuondoka kabisa kwenye eneo hilo. Uchaguzi huo ulionekana kutawaliwa zaidi na jazba kwa wanachama ambao walikuwa wakipinga utaratibu uliokuwa ukitumiwa kwenye upigaji wa kura.

Katika uchaguzi huo uliosimamiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), Amin Bakhresa ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, baadhi ya wanachama walirudia kupiga kura zaidi ya mara moja.

Hiyo ilitokana na utaratibu uliokuwa ukitumiwa katika upigaji wa kura hizo ambapo wanachama walikuwa wakitakiwa kukaa kwenye viti vyao kabla ya kupewa karatasi na kwenda kupiga kura kisha wanachovya kidole katika wino kuashiria kuwa wamepiga kura.

Gazeti hili lilishuhudia baadhi ya wanachama walipopewa karatasi na kupiga kura, hawakuchovya wino vidole vyao na kisha kwenda upande wa pili kuchukua tena karatasi nyingine na kupiga tena kura.

Hali hiyo iliamsha hasira kwa wanachama ambao wengi wao walianza kufanya vurugu wakipinga utaratibu huo, hali iliyosaabisha Polisi kuingilia uchaguzi huo.

Baaada ya askari kuingilia uchaguzi huo, waliwaamrisha wanachama kukaa katika viti kabla ya kuendelea kwenye upigaji wa kura, lakini hata hivyo ilishindikana na ikabidi uanze utaratibu wa kupiga kura kwa kwenda mbele huku wengine wakisubiria kwa muda mrefu bila ya kupewa karatasi ya kupigia kura.

Awali, kabla ya upigaji wa kura haujaanza, Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Ismail Aden Rage aliwaambia waandishi wa habari kuwa anajivunia kumaliza uongozi wake akiwa ameimarisha mifumo mizuri ya klabu.

Mbunge huyo wa Tabora Mjini (CCM) ambaye hakuwania tena kiti hicho, alisema ameiacha klabu ikiwa imejiimarisha vyanzo vyake vya uchumi na ameacha eneo kwa ajili ya ujenzi wa uwanja.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ...

foto
Mwandishi: Evance Ng'ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi