loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Azam FC, El Merreikh robo fainali ya Kagame

Kutokana na ushindi huo, Azam FC imefikisha pointi nane katika Kundi A baada ya mechi zake tano. Ilitoka sare ya 0-0 na wenyeji Rayon Sport, ikaishinda KMKM mabao 4-0, ikalazimishwa sare ya mabao 2-2 na Atlabara ya Sudan Kusini kabla ya ushindi wa leo.

Kwa matokeo hayo, imeshika nafasi ya pili nyuma ya Rayon Sport ambayo jana iliifunga Atlabara bao 1-0 na kufikisha pointi 10.

Hivyo, kwa kuwa washindi wa pili, Azam FC itawakabili washindi wa pili wa Kundi C ambayo ni El Merreikh ya Sudan katika robo fainali. Aidha, Rayon Sport itacheza na mshindi wa pili wa Kundi B ambalo linamaliza mechi zake leo.

Katika mchezo wa jana uliotawaliwa na mashambulizi ya zamu, mabao ya Azam FC ambayo inashiriki baada ya Yanga kufukuzwa na waandaaji kwa kutuma majina ya chipukizi, yalifungwa na John Bocco, Didier Kavumbagu, Mcha Khamisi na Kipre Tchetche. Vijana hao wa Chamazi walikuwa wa kwanza kufunga katika dakika ya 29 baada ya Bocco kutumia krosi ya Mcha kabla ya Desaleny Desta kuisawazishia Adama dakika ya 39.

Hadi wanakwenda mapumziko, timu hizo zilikuwa katika sare ya bao 1-1. Baada ya kurudi kipindi cha pili, Azam ilifunga bao la pili dakika ya 55 lililofungwa na Kavumbagu baada ya kupata krosi ya Erasto Nyoni aliyeng’ara na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.

Timu hiyo iliendelea kushambulia wapinzani wao kwa kasi na kupata bao la tatu lililofungwa dakika ya 60 na Mcha baada ya Kipre kutoa krosi kwa Kavumbagu na kuupeleka nyavuni ambao ulitemwa na kipa wa Adama na kupokewa na Mcha aliyeuzamisha.

Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Adama walioonekana kuchoka kwa kadiri muda ulivyosogea na kukubali bao la nne baada ya dakika ya 75, Kipre kupata pasi ya Nyoni na kuutumbukiza nyavuni.

Bocco anaongoza katika ufungaji baada ya kufikisha mabao matatu akiwaacha nyuma wachezaji wengine wanane wenye mabao mawili, akiwamo Kavumbagu.

Azam FC iliwakosa baadhi ya nyota wake kama Shomari Kapombe, Lionel Saint Preux na Himid Mao ambao ni majeruhi. Mabingwa hao wa Bara watacheza robo fainali Jumanne au Jumatano ijayo kutegemea na matokeo ya mechi ya jana jioni kati ya Rayon na Atlabara ambazo zote zimefuzu kwa robo fainali.

Polisi Rwanda na El Merreikh zimefuzu robo fainali kutoka Kundi C huku mabingwa watetezi, Vital’O ya Burundi ikivuliwa ubingwa baada ya sare na timu hiyo ya Sudan katika mechi ya mwisho juzi.

Tayari Vital’O, Benadir ya Somalia, KMKM, Adama na Telecom ya Djibouti zimeaga michuano hiyo inayofikia tamati wiki hii. Hatua ya makundi inamalizika leo.

MSANII wa Kizazi Kipya, Beka Flavour ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi