loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Azania wazindua Akaunti ya Dhamira

Akizindua akaunti hio jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Charles Singili alisema lengo la akaunti hiyo ni kujenga tabia kwa wananchi ya kujiwekea akiba itakayowawezesha kutimiza malengo yao.

Kiasi cha kufungua akauni hiyo ni Sh 50,000 na mteja anatakiwa kila mwezi kuweka Sh 50,000 au zaidi na hatatakiwa kutoa fedha kwenye akaunti hiyo kwa kipindi cha chini ya mwaka mmoja.

"Tunataka watu wajenge tabia ya kujiwekea akiba, kama una jambo unataka kulifanya mwakani, unafungua Akaunti yako ya Dhamira leo, na kuweka fedha hadi mwaka mmoja unapita unakuwa una akiba ya kutosha kufanya jambo hilo,” alisema Singili.

Aidha alisema ubora wa akaunti hiyo ni kwamba haina makato ya gharama ya kila mwezi, na kwamba mteja anapoweka fedha zake, anapata riba ya asilimia nane na pia akiba hiyo inakuwa dhamana ya mteja kuomba mkopo katika benki hiyo.

"Tunapenda wananchi wote watumie akaunti hii mpya ambayo ipo kwenye matawi yetu yote nchini kwani inatimiza malengo yao, kama ni ada, kununua kiwanja au gari au pengine kulipa ada ya shule," alisema Singili.

MCHICHA ni aina nyingine za ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi