loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Barabara za lami zafikia asilimia 58’

Aidha, serikali imesema ipo haja kwa wahandisi washauri kuwa wazalendo na kuandaliwa vizuri, kuangalia mikataba inayotakiwa imekaaje na kama kuna maeneo yenye hasara, basi yaondolewa ili kuongeza faida.

Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Musa Iyombe, jijini Dar es Salaam jana wakati akifungua mkutano wa Chama cha Wahandisi Washauri Duniani (FIDC).

Alisema uchumi wa Tanzania unatarajia kuwa mzuri, kutokana na kupatikana kwa rasilimali mbalimbali kama vile gesi, makaa ya mawe na urani na ni wazi kuwa kutakuwepo na miradi mingi yenye kuleta maendeleo ambayo itakuwa ikisimamiwa na wahandisi kwa upande mmoja.

Alisema wanaofanya miradi mingi ya ujenzi nchini ni wahandishi washauri kutoka nje ya nchi ambapo kwa kutumia chama cha kishauri ni fursa nzuri watanzania kuweza kuingia na kusimamia na kufanya kazi kizalendo.

Alisema kwa msingi huo, wahandisi washauri wanapaswa kuwa na ujuzi na kutumia mfumo sahihi wa FIDIC kwa kupitia fomu za mikataba na kuona kama kuna maeneo yanayotakiwa kubadilishwa.

“Uchumi wetu unatarajiwa kuwa mzuri kutokana na kupatikana kwa gesi asilia na hata urani miradi mingi ya maendeleo itakuwepo,” alisema Iyombe na kuongeza ni vyema wahandisi washauri wakaandaliwa vizuri.

Rais wa Chama cha Wahandisi Washauri kutoka Tanzania (ACET), Ray Seng’enge alisema FIDC inasaidia wahandisi washauri kusimamia kazi zao kumnufaisha mlaji wa mwisho.

“Mtanzania ndio mlipaji kodi wa mwisho hivyo anahitaji barabara nzuri na huduma nzuri pia... hivyo kwa wahandisi washauri kutekeleza vyema miradi ya maendeleo ni fursa kwao kukuza uchumi,” alisema.

Aidha, alisema ili kazi za kihandisi ziwe na ufanisi, ni wajibu wao wenyewe na sekta binafsi ndiyo wana majibu sahihi, ikiwemo kupunguza bei kwanizinakuwa juu.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kondoa kwa tiketi ya Chama ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi