loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Barcelona inaweza kutumia euro mil 120 kusajili

Kwa sasa Barcelona wapo sokoni kutafuta golikipa mpya na beki wa kati, kwani Victor Valdes na Carles Puyol wanaondoka mwishoni mwa msimu huu na Ofisa huyo amesisitiza kwamba hali yao ya kifedha haitaweza kuwabakiza kipindi cha majira ya joto.

"Kila mwaka tunaangalia tunachoingiza, kodi na kile kinachobaki kama faida na sasa tuna kama euro milioni 120," Bartomeu aliliambia gazeti la El Periodico.

"Kwa kawaida huwa tunatumia nusu ya fedha hizo kwa ajili ya kuingiza kwenye soko la kutafuta wachezaji na pia kupunguza madeni yetu.

"Lakini kuna mwaka mwingine tutalazimika kutumia fedha zote euro milioni 120 kwa ajili ya usajili wa wachezaji."

Barcelona wanatarajia kumtangaza kipa wa Borussia Monchengladbach, Marc-Andre ter Stegen kuwa golikipa wao mpya hivi karibuni, huku pia wakiwa wanahusishwa na kutaka kuwasajili David Luiz, Jan Vertonghen na Eliaquim Mangala kwa ajili ya kuimarisha safu yake ya ulinzi.

TIMU ya soka ya Polisi Zanzibar inayoshiriki Ligi Kuu ya ...

foto
Mwandishi: BARCELONA, Hispania

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi