loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Barclays yazindua kampeni mpya

Licha ya kuzindua kampeni hiyo, benki hiyo jana hiyo ilichezesha bahati nasibu ya kwanza kwa wateja wake, ambao walishaanza kushiriki katika kampeni hiyo, ambayo ilitangazwa na benki hiyo Septemba mwaka huu.

Wateja watano walishinda kwenye bahati nasibu hiyo. Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Kawaida wa benki hiyo, Musa Kitoi, kampeni hiyo itawapa fursa wateja watano kila mwezi kujishindia mpaka kiasi cha Sh milioni moja kila mmoja katika kipindi chote chote cha kampeni hiyo.

Kitoi alisema mwisho wa kampeni hiyo ni Januari mwaka kesho, ambako mshindi wa jumla atapatikana na atazawadiwa Sh milioni 30. Droo ya kampeni hiyo itakuwa ikifanyika katika kila wiki ya mwisho wa mwezi, ikiangalia vigezo vya kila mteja.

"Kampeni hii iko wazi kwa wateja wote wa Barclays na wale wapya kupitia akaunti zao mbalimbali za fedha za Tanzania," alisema Kitoi.

Aliongeza kuwa ili mteja aweze kushiriki lazima aweke kiasi cha fedha kisichopungua Sh 300,000. Kiasi hicho kinatakiwa kiwekwe ndani ya mwezi kutoka kampeni hiyo izinduliwe na inatakiwa katika akaunti zao, kiasi kama hicho kisishuke.

Alisema wateja wapya wanaweza kuingia kwenye droo hiyo pindi tu watakapofungua akaunti zao na kuweka kiasi kama hicho.

Kwa droo iliyofanyika jana walioshinda ni Azani Omari, Severine Rweba, James Allan, Barik Mwasaga na Ipyina Lazaro. Kitoi alisema benki itaangalia kiasi cha wateja hao walichoweka na kisha watawawaekea zawadi zao.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi