loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Basi laua 4, kibaka achomwa akiibia majeruhi

Basi hilo, mali ya kampuni ya Wibonela, linalofanya safari zake kati ya Kahama na Dar es Salaam, lilipinduka jana majira ya saa 12 asubuhi mjini hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na alitembelea Hospitali ya Wilaya ya Kahama kuwajulia hali majeruhi.

Aliagiza kufanyike msako mkali wa dereva, Godfrey Prochas aliyesababisha ajali na kutoroka eneo la tukio.

Alisema basi hilo aina ya Scania lenye namba za usajili T 412 CGN, lilipata ajali kutokana na mwendo kasi na uzembe wa dereva katika eneo la Phantom Kata ya Nyasubi, likiwa linaanza safari ya kuelekea Dar es Salaam.

Aidha, mashuhuda wa tukio hilo walisema dereva wa basi hilo, alikuwa anashindana na mabasi mengine ili kuwahi eneo la mizani kupima uzito.

Lakini, kutokana na mwendo kasi, alipojaribu kuingia barabara kuu akitokea kituo cha mabasi, lilimshinda na kuserereka na kisha kuangukia mtaroni lilikopinduka matairi yote yakiwa juu.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama, Dk Joseph Ngowi alithibitisha kupokea maiti nne za ajali ya basi, ikiwemo moja ya mtoto mwenye umri wa miezi mitatu, Robineck Jordan na mwanamke mjamzito aliyefahamika kwa jina la Amina, mkazi wa Kigoma.

Mwingine ametajwa kwa jina moja la Salum (35-40) na mwingine hakufahamika, lakini anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 40-45. Pia, alisema amepokea majeruhi 40, huku wanne hali zao zikiwa mbaya.

Alisema kwamba utaratibu unaandaliwa waweze kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi

UDANGANYIFU wa kitaaluma ambao hujikita katika aina nyingi na nyanja ...

foto
Mwandishi: Raymond Mihayo, Kahama

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi