loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Batuli na mtazamo wa filamu za kimataifa

Nyota huyo alishawahi kufanya kazi nzuri katika filamu ya Fungate, Glory of Ramadhani, Waves of Sorrow huku akishirikiana na wasanii Kama Steve Mangele ‘Steve Nyerere’ Vicent Kigosi ‘Ray’, marehemu Steven Kanumba, Issa Mussa ‘Cloud 112’ na wasanii wengine kibao ambao ameshafanya nao kazi.

Batuli anasema kwa muda mrefu alikuwa akitumikia filamu za watu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutambuliwa na kujulikana zaidi. Lakini anasema kikubwa alikuwa hajakamilika katika kufanya kazi zake mwenyewe hususani katika upande wa bajeti kwa kuwa hakutaka kufanya kazi zilizopoa na kudorora.

Kwa sasa nyota huyo ambaye ana umaarufu mkubwa, anasema amejipanga kuachia filamu zake tatu tofauti, ambazo pia ni filamu zake za mwanzo chini ya uongozi wake mpya. Anasema tangu alipoingia mkataba na meneja huyo mpya, zaidi ya miezi miwili iliyopita hivi sasa tayari ameshaanza kuandaa filamu tatu mfululizo pamoja na matangazo ya televisheni.

Batuli anasema filamu yake ya kwanza inaitwa Wekeza Inalipa, ambayo pia ameifanyia kipindi katika moja ya vituo vya stesheni za televisheni ili kuhamasisha watu kuwekeza hasa katika hisa. “Katika filamu hiyo huwa nazungumzia umuhimu wa watu wa kununua hisa, ni moja ya filamu zangu za tofauti sana na nzuri kwa mimi naikubali sana,” anasema msanii huyo.

Filamu hiyo anasema imeambatana na matukio ya mbalimbali ya kutoa elimu na kuwafunza watu wajali zaidi maisha ya baadaye hasa kwa kununua hisa zinazoweza kusaidia maisha yao kupambana na umasikini. Zaidi ya filamu, anasema pia amefanya kipindi akiwa kama mtangazaji katika moja ya stesheni ambazo zitakuwa zikionesha filamu hiyo ya Wekeza Inalipa.

Filamu yake ya pili anasema kwa sasa ndiyo ipo kwenye mikakati ya mwisho katika uchanganyaji wa picha ambao ameshirikiana na wasanii kutoka Afrika Mashariki na Kati. “Kwa sasa bado sijaruhusiwa kuwataja wala kutaja jina la filamu kwa kuwa bado tupo kwenye mkakati wa kuhakikisha inaisha na kuitangaza kabla ya kuingia sokoni,” anasema Batuli.

Anasema kazi hizo zote zinampa moyo juu ya matarajio yake ya kuwa miongoni mwa wasanii wakubwa wa Afrika Mashariki na Kati na Afrika nzima katika suala zima la filamu. “Tunaelekea vizuri katika kazi nzuri ya filamu ambao itawezesha wasanii kufika mbali hususani kutokana na malengo yetu,” anasema.

Batuli anasema hivyo amejipanga zaidi kufanya filamu zenye stori nzuri na zenye mvuto kuanzia mavazi hadi waigizaji ili kupamba na soko la kimataifa kuliko kuangalia zaidi soko la ndani. Kuhusu kuwa na meneja, anasema maamuzi yake ya kutafuta meneja kwa ajili ya kazi yake, si kwamba alikurupuka kuwa na meneja ilimradi meneja, la hasha.

Isipokuwa alifikiria na kuamua kutafuta meneja ambaye anaweza kusimamia kazi yake na kumfikisha katika kiwango cha kimataifa zaidi. Anasema wasanii wengi wamekuwa wakihangaika wenyewe bila ya kuwa na uongozi au meneja atakayeweza kusimamia vizuri kazi zake, kwa tena kwa sheria za nchi.

“Anasema wasanii wengi wamekuwa hawana elimu ya kutosha kuhusiana na usimamizi wa kazi zao, na ndio maana wamekuwa wakiburutwa bila ya kujua washike wapi,” anasema. Hivyo kwa msanii kuwa na meneja kutamsaidia baadhi ya kazi zake za sanaa kuwa chini ya usimamizi mzuri, bila ya msanii kuathirika na chochote.

Anasema mara nyingi wasanii wengine wanatafuta meneja ambaye hawezi kumsaidia isipokuwa meneja ndiyo anamtegemea msanii. Anasema meneja ni lazima aijue biashara ambayo anaenda kuiwekeza na kujua hasara na faida ya kazi yake. Kufanya hivyo kutamwezesha kuweza kufika mbali, kwa msanii na meneja mwenyewe.

“Kama ninakuwa na wazo la simulizi ya filamu, huwa nalifikisha kwa meneja wangu ambaye naye anakuwa na watu wake kwa pamoja wanaiangalia na kuniambia na baadaye kufanya kazi baada ya kuona inafaa,” anafafanua zaidi. Anasema hiyo ndiyo kazi kubwa ya meneja wake na kama kuna lingine basi huwa wanakaa chini na kujadiliana, ili kufika mwafaka.

Kwa sasa Batuli anasema lengo lake ni kufika katika anga za filamu za kimataifa zenye kiwango cha juu, ikiwemo kuwashirikisha waigizaji kutokana na wenye uwezo mkubwa wa kuigiza. Kwa muda wa miezi miwili tangu aingie mkataba na meneja huyo, anasema tayari ameshaanza kuona mafanikio makubwa ambayo anaamini yatamwezesha kufika mbali zaidi.

Amesema hapendezwi na wasanii wanaovaa nguo fupi na zenye kuonesha sehemu ya maungo yao. Anasema kuvaa nguo za namna hiyo, sio kwamba wanaweza kusaidia kazi zao kuuzika, ila wanajidhalilisha kutokana na Watanzania sasa wamebadilika na wanaangalia kazi zaidi. Anasema licha ya umaarufu, lakini hajalewa sifa na ndiyo maana ameamua kujikita zaidi katika filamu za kiwango cha juu.

“Siku hizi watu hawaangalii unavaaje? Au mzuri kwa kiasi gani isipokuwa wanaangalia kazi yako ipo vipi,” anasema. Mama huyo wa mtoto mmoja, Abdul, aliyeanza kuigiza mwaka 2008 katika filamu ya Mkasa, anasema kwa sasa nguvu zake zote ameamua kuwekeza kwenye kazi zake mpya ili kufanikiwa na kujenga jina kubwa.

"The Game Changer: President Magufuli's First Term in Office" ...

foto
Mwandishi: Mohamed Mussa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi