loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Beki za Azam, Mbeya City kiboko

Wakati Yanga ikiongoza kwa kufunga mabao 28 nyavuni kwa michezo 12 iliyokwishacheza, Mgambo JKT kutoka Tanga inashika mkia kwa kuwa timu iliyofungwa mabao mengi zaidi ikiwa imefungwa mabao 21 na kufunga mabao matatu katika michezo 12 iliyocheza.

Azam FC yenye maskani yake Chamazi jijini Dar es Salaam na Mbeya City kutoka jiji la Mbeya ndizo timu pekee ambazo hadi sasa zimeonesha kuwa na beki imara, kwani zimeruhusu nyavu zao kutikiswa mara 7 tu huku zikiwa hazijapoteza mchezo hata mmoja na ndizo zinaongoza ligi hiyo Azam ikiwa ya kwanza kwa tofauti ya magoli ya kufunga, zote zina pointi 26.

Na timu hizi zitakutana katika mechi ya mwisho kesho kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, mechi inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.

Aidha katika msimamo huo wa ligi timu za jeshi za JKT Ruvu na Mgambo ndio zinazoongoza kwa kupoteza michezo, zimefungwa mechi nane kila moja huku Wagosi wa Kaya Coastal Union wakiongoza kwa kutoka sare michezo 7 ikifuatiwa na Simba yenye sare 6 kati ya michezo 12 iliyokwishakucheza.

Katika mlolongo huwa mchezaji Amis Tambwe wa Simba anaongoza kwa kuwa mtikisa nyavu bora hadi sasa baada ya kuchungulia nyavu za timu pinzani mara 9.

Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu soka Tanzania bara unataraji kumalizika kesho na keshokutwa na tayari timu za Azam na Mbeya City ambayo ni ngeni katika ligi hiyo zimeshaichachafya miamba ya soka la Tanzania Simba na Yanga.

MCHEZO wa Ligi Kuu ya Soka la Wanawake kati ya ...

foto
Mwandishi: Mroki Mroki

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi