loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Benchi la ufundi Simba kuvunjwa

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya Simba, uongozi wa timu hiyo hauko tayari tena kukubali matokeo yasiyoridhisha.

Simba imekuwa ikiongoza ligi kwa muda mrefu tangu kuanza kwa mzunguko wa kwanza, lakini katika mechi za karibuni ilianza kupata matokeo ya sare, hali inayozusha mtafaruku ndani ya timu hiyo.

Simba kwa sasa iko nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 21 na hata kama itaifunga Ashanti kesho haitaweza kurudi tena kileleni kwani itafikisha pointi 24 wakati Yanga inayoshika nafasi ya tatu kabla haijacheza mechi yake ya mwisho ina pointi 25.

Mechi ya mwisho ilikuwa wiki iliyopita dhidi ya Kagera Sugar na kutoka sare ya bao 1-1, hali iliyopelekea kutokea kwa vurugu za mashabiki wakivunja viti na baadhi yao wakilalamika waamuzi kutowatendea haki.

“Kwa kweli uongozi hautovumilia kuendelea kupata matokeo mabaya, salama ya benchi la ufundi ni kushinda mechi ya mwisho lakini timu ikitoka sare au ikifungwa, benchi lote litavunjwa,” alisema mtoa habari hiyo.

Benchi la ufundi la Simba linaongoza na kocha Mkuu Abdallah Kibadeni akisaidiwa na Jamhuri Kihwelo, ‘Julio’. Wakati huo huo, Simba imeingia kambini jana kwenye hoteli ya Bamba Beach Kigamboni, kwa ajili ya kujiandaa na mechi dhidi ya Ashanti United.

Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema jana kuwa wachezaji 26 watakuwepo kwenye kambi hiyo ambapo baadhi yao waliokuwa hawajachaguliwa katika mechi mbili zilizopita wamerejeshwa kikosini.

Wachezaji hao ni Henry Joseph na Ramadhan Chombo ambao watakuwepo katika mechi hiyo huku Haruna Chanongo akiwa bado hajarejeshwa kundini wakati Nassoro Masoud ‘Cholo’ ni majeruhi wa nyama za paja na Zahoro Pazi akiugua malaria.

MCHEZO wa Ligi Kuu ya Soka la Wanawake kati ya ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi