loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bendera mgeni rasmi michezo wa Mei Mosi

Katika mchezo huo, Mabingwa watetezi wa mwaka jana kwa upande wa mpira wa miguu, timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani itapambana na Timu ya Kuchambua na Kusindika Tumbaku (TTPL) ya Morogoro kwenye mechi ya ufunguzi.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa kamati ya michezo hiyo, Award Safari alipozungumza na waandishi wa habari. “Kwa upande wa netiboli, mabingwa watetezi kutoka Wizara ya Ulinzi watapambana na Shirika la Mzinga".

Safari alisema kamati ya mashindano hayo imeongeza muda wa timu kuthibitisha ushiriki ambapo sasa zitatakiwa kufanya hivyo mpaka Aprili 11 badala ya Machi 30 kama ilivyokuwa awali.

Alisema, timu 14 zimethibitisha kushiriki mpaka sasa ambazo ni Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Polisi Tanzania, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu (CDA) Dodoma, Kampuni ya Tumbaku (TTPL) ya Morogoro, Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) na Wizara ya Uchukuzi.

Nyingine ni Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Afya, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mahakama Kuu ya Tanzania, Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ( SUA).

“Timu zinazotoka nje ya Mji wa Morogoro zinatakiwa kufika Morogoro Aprili 14 mwaka huu, na michezo itakayoshindaniwa ni soka, netiboli, kuvuta kamba, kukimbia mbio ndefu, baiskeli, karata, bao na drafti,’’ alisema Safari.

Aidha, mwenyekiti na katibu katika kila timu, wanakumbushwa kuhudhuria mkutano kati yao na kamati inayosimamia michezo hiyo Aprili 15 mwaka huu, saa nne asubuhi kabla ya mkutano wa wanamichezo wote utakaofanyika saa 10 jioni ya siku hiyo.

TIMU ya soka ya Polisi Zanzibar inayoshiriki Ligi Kuu ya ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi