loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Benki Kuu yaboresha Makumbusho ya Nyerere

Msaada huo ulitolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kuimarisha shughuli za uhifadhi wa vifaa mbalimbali vilivyokuwa vikitumiwa na Baba wa Taifa.

Hafla hiyo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa maonesho ya sarafu na noti zilizoanza kutumika nchini tangu mwaka 1967, ikiwa ni moja ya shughuli kama mchango wa benki hiyo katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Nyerere yanayoadhimiswa nchini kila ifikapo Oktoba 14.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Juma Reli ambaye ni Naibu Gavana wa BoT alisema Nyerere anakumbukwa kwa mambo matatu ambayo ni uzalendo, utu na kujitegemea, aliyowaachia Watanzania.

Naye Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa, Profesa Audax Mabulla, alishukuru kwa msaada huo kutoka Benki Kuu ya Tanzania na kwamba wameupokea kwa furaha na kuongeza kuwa ufadhili huo ni wa kuunga mkono juhudi za kukusanya na kuhifadhi vifaa mbalimbali vya Baba wa Taifa na mchango wa kitaifa na kimataifa.

Akishukuru kwa niaba ya Serikali, Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Angelina Mabula, alisema msaada huo si mdogo na kwamba kwa niaba ya Serikali anatoa shukrani za dhati kwa benki hiyo.

Mabula aliwaomba wadau mbalimbali ambao wanawiwa na kuchangia na kuenzi uhifadhi wa kumbukumbu za Mwalimu ambazo ni historia ya Taifa waige mfano huo.

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza bidhaa ...

foto
Mwandishi: Ahmed Makongo, Butiama

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi