loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Benki ya Dunia, Hazina watiliana saini

Mikataba hiyo imesainiwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk Servacius Likwelile na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Philippe Dongier.

Katibu Mkuu Likwelile alisema miongoni mwa fedha hizo, Sh bilioni 537.9 zitatumika kwa ajili ya kuendeleza jiji la Dar es Salaam.

“Mkopo huu unalenga kuboresha huduma za mijini na kuimarisha uwezo wa taasisi katika jiji la Dar es Salaam,” alisema na kuongeza kuwa kipaumbele kitatolewa kwenye miundombinu kama kwenye barabara zinazotumika na kudhibiti mafuriko.

Alisema mkopo wa pili wa Sh bilioni 107.6, utaendeleza ujenzi wa nyumba za gharama nafuu. Likwelile alisema fedha hizo zitapewa taasisi za fedha kwa ajili ya kukopesha wenye uhitaji wa nyumba.

Alisema Sh bilioni 64.5 ni kwa ajili ya mradi wa uvuvi wa kikanda, katika nchi za Tanzania, Comoro na Msumbiji.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi