loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Benki ya Exim yaadhimisha miaka 17

Sambamba na hilo imebuni mpango mpya ujulikanao kama ‘innovative retail model’ utakaosaidia kuboresha mawasiliano kwa wateja na uratibu wa matawi katika maeneo ya kazi.

Meneja Mwandamizi wa benki hiyo tawi la kwanza kufunguliwa nchini mwaka 1997, Nancy Huggin, alisema ustawi wa benki hiyo unatokana pia na ushirikiano wao na jamii.

Alisema sasa wamejikita katika mpango huo wa kibunifu, kusaidia kuboresha mawasiliano kwa wateja. Sherehe za maadhimisho hayo zilifanyika Ijumaa iliyopita jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na wateja nchi nzima.

Exim ina matawi 27 ndani na nje ya nchi. Mkuu wa Idara ya Uendeshaji na mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu wa benki hiyo, Eugene Masawe alisema benki ya Exim imekuwa na mpango kazi madhubuti wa ‘upanuzi na ugunduzi’ tangu kuanzishwa kwake kama benki ya Kitanzania.

Alisema mali zake kwa jumla zimevuka Sh trilioni moja ilipofika Juni mwaka 2013 na kwamba lengo ni kuboresha zaidi huduma kwa ustawi wa jamii na kuifanya kuwa benki bora kuliko zote nchini na nje.

Alisema wakati faida ghafi ya benki ikikua kwa asilimia 80 (Sh bilioni 9.6), pato la jumla litokanalo na riba limekua kwa asilimia 36 (Sh bilioni 14.3) na pato kupitia biashara ya fedha za kigeni, liliongezeka kwa asilimia 33 kuanzia mwaka jana na kwamba hivyo ni viashiria thabiti kwamba benki hiyo itafikia malengo katika miaka michache ijayo.

Kwa upande wake, Kaimu Ofisa wa Fedha Mkuu wa Exim, Issa Hamisi, alisema, “kipaumbele chetu kikubwa kinabaki kuendelea kuimarisha nafasi yetu katika soko na kuboresha ufikiwaji wa matakwa ya mteja kupitia utendaji ulio na ufanisi.”

KAMPUNI ya uchimbaji ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi