loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Benki ya Posta wakabidhi vifaa vya usafi

Msaada huo umetolewa baada ya uongozi wa soko la Feri kupeleka maombi kwa uongozi wa benki hiyo kuomba kusaidiwa vifaa vya kufanyia usafi.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya Posta, Sosthenes Nyenyembe alisema kuwa vifaa walivyonunua ni pamoja na mapipa ya kuhifadhia taka, makoleo, mafagio na matoroli.

Alisema soko hilo kwa siku linaingiza watu zaidi ya 7,000 kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo watalii wanaokuja kwa ajili ya shughuli mbalimbali nchini.

Nyenyembe alisema kuwa wataendelea na utaratibu wa kusaidia masuala ya maendeleo ikiwa ni njia mojawapo ya kurejesha faida wanayoipata kutoka kwa wateja wao.

Ofisa Masoko wa Manispaa ya Ilala, Athumani Mbelwa aliupongeza uongozi wa benki hiyo kwa msaada waliowapatia na kutaka taasisi nyingine kuiga mfano huo.

Mbelwa alisema kuwa vifaa hivyo vitawasaidia kwa kiasi kikubwa katika shughuli za ukusanyaji wa taka zinazotokana na samaki katika soko na kuondoa mrundikano wa taka pindi gari linapokosekana.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi