loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Benki yakopesha wanawake bil. 20/-

Mkurugenzi Mwendeshaji wa benki hiyo, Margreth Chacha, aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kuwa katika kipindi cha chini ya miaka minne tangu benki hiyo ianzishwe, maelfu ya wajasiriamali wanawake na vijana wameshanufaika na mikopo ya kuendeleza biashara zao.

“Mikopo yetu kwa wajasiriamali hawa imekuwa kichocheo kikubwa katika kupanua wigo wa biashara zao hapa nchini na marejesho ya mikopo hiyo kutoka kwa wajasiliamali na vijana, inaridhisha na kutia moyo,” alisema Margreth.

Margreth alisema benki hiyo imeona kwamba kuwawezesha wajasiriamali wanawake na vijana, kuna maana kubwa sana katika kuchangia maendeleo na ukuaji wa shughuli za kijamii na uchumi nchini.

“Ni imani ya benki kuwa wanawake na vijana ni wachangiaji wakubwa katika uchumi wa nchi, kwani wao idadi yao ni kubwa hivyo endapo watawezeshwa vilivyo, watasimama katika nafasi kubwa ya kubadilisha uchumi,” alisema.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mwendeshaji huyo, Sh bilioni 17.6 zimetolewa kwa wajasiliamali na vijana kwa Mkoa wa Dae es Salaam, Sh bilioni 1.3 kwa wajasiriamali wa Dodoma na Sh milioni 686 kwa wajasiriamali wa Mwanza.

“Wakati sasa tukiwa katika mpango kamambe wa kujitanua kila sehemu hapa nchini, tayari benki yetu imeshatoa mikopo ya Sh milioni 178 kwa wajasiriamali na vijana mkoani Mbeya na Sh milioni 366 kwa wajasirialiamali vijana mkoani Ruvuma".

Margreth aliongeza kuwa wajasiriamali wanawake na vijana katika mikoa hiyo, wamenufaika na mikopo iliyotolewa na benki na pia biashara zao zinaendelea vizuri.

“Wajasiriamali katika Mkoa wa Dodoma walijiunga katika vikundi na mikopo yao waliitumia kununulia mashine za kukamulia mafuta ya alizeti, ambapo wale wa mkoani Mbeya walielekeza katika ununuzi wa matrekta madogo ya kulimia maarufu ‘power tillers’,” alisema.

KAMPUNI ya uchimbaji ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi