loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Biashara ya ndizi yawekewa utaratibu

Hatua hiyo inafuatia Halmashauri ya Wilaya hiyo, kukamilisha ujenzi wa Soko la Kijiji cha Kitandu, Tarafa ya Kibosho na kuweka utaratibu maalumu wa jinsi ya kuendesha biashara hiyo ikilinganishwa na hali ilivyokuwa awali.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Morris Makoi alisema soko hilo limegharimu zaidi ya Sh milioni 30, na kwamba kuanzia sasa utaratibu wa kuuza ndizi mitaani umefutwa na wafanyabiashara watatakiwa kulitumia soko hilo kuuza mazao yao.

"Awali wafanyabiashara walikuwa wakiuza mazao yao huko mitaani, halmashauri imeamua kujenga soko hili ili kutengeneza mazingira mazuri zaidi ya kibiashara ili sote tunufaike, wafanyabiashara kwa upande mmoja na halmashauri kwa upande mwingine,” alisema.

Makoi alisema uongozi wa soko hilo utakuwa unawasiliana moja kwa moja na masoko kama ya Dar es Salaam na mikoa mingine juu ya biashara ya ndizi katika masoko hayo ili wakulima wauze kwa bei itakayopatikana na kulifanya zao hilo kuwa la biashara na faida kwa wakulima.

Kwa upande wao, mmoja wa wananchi wa kijiji hicho, Elirehema Moshi katika risala ya uzinduzi wa soko hilo, alisema litakuwa la kila siku kwa mazao na bidhaa mbalimbali ambapo wafanyabiashara watatozwa ushuru wa wastani wa Sh 200 na Sh 500 kwa siku.

Walisema fedha hizo zitasaidia kuongeza pato la kijiji na halmashauri ya wilaya hiyo, na sehemu ya fedha zitatumika kuboresha huduma nyingine muhimu ikiwamo miundombinu ili kusafirisha mazao kwa uhakika zaidi.

Akizindua soko hilo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Dk Ibrahim Msengi, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Remda Ibrahimu aliitaka halmashauri hiyo kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana ikiwa ni pamoja na mazingira mazuri ya kibiashara.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi